MAFUNDISHO YA LUGWILA:TAZAMA, UNAPANDA KWENDA YERUSALEMU!




Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii.
      [Luka 18:31]

Yesu, akiwa anajua yuko katika nyakati za mwisho za yeye kuwa duniani, aliwaambia wanafunzi wapande kwenda Yerusalemu.

Sababu ya kwenda Yerusalemu ilikuwa ni ili mambo yote yaliyoandikwa kuhusu yeye yakatimizwe.

Tuangalie sifa kidogo za mji huu wa Yerusalemu!!!


      {Luka 13:34}
Ee Yerusalemu, Yerusalemu,  uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka.

Wakazi wa Yerusalemu, yaani wayahudi, walikuwa na kawaida ya kuwakataa watumishi wa Mungu na kuwaadhibu wapelekao ujumbe wa Mungu.

Ukiangalia vizuri, kwa watumishi wa Mungu, Yerusalemu haukuwa sehemu salama hata kidogo, kwani, ungefika hapo, ilimradi tu ni mtumishi wa Mungu, wangekutesa vilivyo.

Yesu, hali akijua mateso yatakayompata, anawaambia wanafunzi, wapande naye kwenda Yerusalemu.

Kwamba, hakukuwa salama lakini kwa sababu ya kutimizwa yale aliyoandikiwa na kwamba haifai nabii kufa nje ya Yerusalemu, anakwenda Yerusalemu!!!

Hatima ya Yesu ilikuwa ni Yerusalemu.
      [Luka 13:33]

Kusudi la Mungu kwa Yesu lilifungwa kwenye neno lake Mungu alilolinena kupitia manabii ili neno hilo litimie.

Kuna hali unapitia au utapitia ili kusudi la Mungu litimie; inaweza kuwa hali ngumu au nzuri, umejiandaaje kutimiza kusudi la Mungu katika hali ngumu au utaikana imani, kwa mfano?

Tazama sasa unapanda kwenda Yerusalemu, huko kuna mateso, kukataliwa, kuonewa, kudhihakiwa na kila aina ya ubaya; _je, uko tayari kuendelea kwa ajili ya Mungu?_ 

Unakwenda kuwashuhudia habari njema watu wa Ninawi ambao wamekuwa watu wa dhihaka na kejeli ili kusudi la Mungu litimie, au unaogopa fedheha?


Unakwenda kukutana na changamoto,, huwezi kukwepa kama ni kusudi la Mungu; unahitaji nguvu za kupita na kuvuka kwenye hiyo changamoto.

 unakwenda Yerusalemu, jipe moyo kwa ajili ya kusudi la Mungu .

 Mwl Lugwila,
+255 756 668 583
 Njoni, vyote vimekwisha kuwekwa tayari.
Tags:

Post a Comment

0 Comments