Kati ya sifa kubwa unayotakiwa kuwa nayo ili uweze kufanikiwa kimaisha ni uwezo wako wa kughairisha (suspend) mambo yanayokupa raha kwa muda mfupi ili kujenga mambo yatakayokupa furaha kwa muda mrefu.
Mwanzoni mwa 1960 Professor Walter Michael wa chuo kikuu cha Stanford alifanya jaribio fulani la tabia ambalo limekua marufu sana miongoni mwa wanazuoni wa sayansi ya jamii na saikolojia. Jaribia hilo linajulikana kama “Marshmallow Experiment”.
Katika utafiti huu aliwajaribu watoto wadogo kama 100 wenye umri wa miaka minne na mitano. Aliwaweka katika chumba na akawawekea kila mmoja kipande cha mkate mtamu wenye chocolate.
Kisha akawaambia “Kama nikirudi nikakuta haujala huu mkate nitakupatia kimkate cha pili, ila kama nikirudi nikakuta umeshakula sitakupatia kitu.”
Kisha akawaacha kwa dakika kumi na tano (15) wakiwa peke yao chumbani halafu akarejea. Aliporudi alikuta matokeo kama ifuatavyo:
1. Zaidi ya watoto 60 walibugia ile mikate baada tu ya yule Profesa kutoka. Yani alipofunga mlango tu wao wakala mara moja ile mikate licha ya ahadi waliyopewa.
2. Watoto 30 walijitahidi kujizuia kwa kujizungusha zungusha lakini mwishoni walikula.
3. Watoto wachache sana (chini ya 10) ndio walioweza kujizuia na kutokula ile mikate kwa dakika zote 15. Watoto hawa waliacha kula wakiwa na matarajio ya kupata mikate ya ziada kama walivyoahidiwa.
Profesa Walter aliwafuatilia watoto hawa kwa muda wa miaka 40 mfululizo na uligundua yafuatayo;
1. Watoto walioshindwa kujizuia walikua na maisha mabovu baadae. Hawakujua umuhimu wa kuweka akiba. Walitumia pesa zote walizopata kwa starehe. Hawakuwa wabunifu na walitegemea zaidi kazi za kuajirdiwa ktk maisha yao yote.
2. Watoto waliojizuia kwa muda mfupi lakini badae wakala hawakua na maisha yenye msimamo. Walipanga mipango ya maendeleo lakini hawakuikamilisha kwa sababu ya hofu ya kushindwa. Baadhi walianzisha biashara lakini zilipoyumba kidogo walirudi kuajiriwa na hawakufanya biashara tena.
3. Watoto ambao walikuwa na uwezo wa kujizuia na hawakula kabisa ile mikate walikuwa na mafanikio makubwa sana kimaisha. Hawakujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya, walikuwa na nidhamu ya fedha na walikuwa waaminifu ktk ndoa zao na maisha kwa ujumla.
Hii inaitwa “The power of delayed gratification” yani nguvu ya kuweza kujizuia vinavyokufurahisha kwa muda ili uweze kufaidi vitu vya muda mrefu katika maisha yako.
MORAL:
Kupitia theory hii ya Prof.Walter tunajifunza mambo mengi katika maisha. Kwa kawaida mambo yanayotuharibia “direction ya maisha” ni yale yanayotupa raha kwa muda mfupi lakini huwa yana madhara mengi kwa baadae.
Kwa mfano; kuangalia “movies” kwa masaa inakupa raha ya muda mfupi lakini ungetumia muda huo kujiendeleza katika ujuzi kwa kusoma au kufanya biashara kungekupa matokeo mazuri na ya muda mrefu.
Kwa kawaida tunapenda kujiachia na kufanya mambo yanayotupa raha ya muda mfupi bila kujali matokeo yake hadi baaada ya miaka mingi sana ndipo tunakuja kujutia. Mwanzoni unaweza kuona kama hakuna madhara yoyote unayopata kwa sasa.
Hujawahi kukaa na wazee wakaanza kukupa story zao walivyokula bata zamani? Watakuambia mahali fulani viwanja vilikua bei Rahisi sana lakini cha ajabu hawakukunua. Kwa wale wazee walioishi Dar enzi hizo ukimkuta atakwambia Segerea ilikua pori, ulikua ukienda na senti 50 ukimpa Mjumbe unajipimia eneo mwenyewe. Lakini yeye bado anaishi nyumba ya kupanga. Unajiuliza mbona yeye alishindwa kujipimia.??
Au anakwambia Mbezi Beach viwanja vilikua vinalingana bei na kreti moja ya bia. Lakini unashangaa yeye hakununua. It means “aliopt” kreti ya bia instead of kiwanja. Maana yake ni kuwa alichagua jambo la kumpa raha muda mfupi lakini akateseka badae muda mrefu.
Uwezo wako wa kujizuia kutonunua nguo za gharama kwa sasa ili kuwekeza ndio utakaokufanya uwe na maisha mazuri kesho. Uwezo wako wa kujizuia kutonunua simu ya gharama kubwa leo ili usave pesa yako kwa badae ndio kiini cha mafanikio yako.
Uwezo wako wa kujizuia kutoishi kwenye nyumba ya gharama kubwa ili utunze pesa ununue kiwanja chako ndio utakaokufanya ujenge kwako na uondokane na nyumba za kupanga.
Kila wakati jitahidi kuwa mtu unayeweza kujizuia kufanya vitu vinavyokupa raha ya muda mfupi ili uweze kujenga msingi wa kupata mafanikio ya muda mrefu maishani mwako.
Leo jiulize ni vitu gani maishani mwako ambavyo vinakupa furaha ya muda mfupi lakini vinakuharibia malengo yako ya muda mrefu? Ukiweza kuvitambua, mara moja dhamiria na anza kuviepuka ili kujenga msingi imara wa mafanikio yako ya muda mrefu.
Kumbuka, kama hautakuwa tayari kuumia kidogo leo ili upate raha ya muda mrefu, utajikuta unapata raha kidogo leo na unaumia maisha yako yote.
Theory hii ya Prof.Walter imenikumbusha Mwalimu wangu wa Chuo Kikuu Prof.Bernadin Mfumbusa ambaye kwa sasa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Kondoa aliwahi kuniambia kuwa kuna falsafa mbili za maisha katika maendeleo “either uteseke sasa ufurahi baadae, au ufurahi sasa uteseke badae”
Akina Bakhresa, Mengi, Dewji walikubali kuteseka kwa muda fulani ili waje wapate raha ya muda mrefu.
Bakhersa aliwahi kusema kuwa alianza biashara yake kama “baba lishe” kwa kuuza mgahawa huko Z’bar. Alikubali kuteseka kwa muda mfupi ili atengeneze kesho yake. Leo Bakhresa ni bilionea. Angeamua “kula bata” kipindi hicho bila shaka asingekuwa hapa alipo leo. Pengine angekua bado anasugua sufuria kule Zanzibar akipikia watu.
Mabilionea wakubwa kama Mark Zukerberg, au Bill Gates leo wana maisha mazuri kwa sababu walikubali kuteseka kwenye “jana yao”.
Sasa wewe umeanza kazi leo unataka “udrive” wakati huna hata mwaka kazini. Unadhani kesho yako itafanikiwa?
Unalipwa “milioni moja” lakini umepanga nyumba ya laki 5 kwa mwezi. Unafurahia watu wakija kwako wanasifia geti la gharama kubwa na kukupamba “unakaa nyumba kali”. Unalewa sifa na kusahau kwamba hilo geti ni la mwenye nyumba na wewe ni mpangaji tu. Aisee my friend Sahau kitu kinachoitwa mafanikio kwako. Utaishia kukaa nyumba za kupanga hadi uzeeni.
Kubali uteseke muda mfupi leo ili ufurahi muda mrefu kesho, au amua kufurahi muda mfupi leo na uteseke muda mrefu kesho. Uamuzi ni wako.!Siku njema.
0 Comments