Zijue faida 5 kufanyiwa tohara kwa wanaume

Tohara ni muhimu sana katika afya ya mvulana yeyote yule, na ndiyo maana hata wizara ya afya ikaona ni vyema kuanzisha hata huduma ambayo itawafanya watu waweze kupewa huduma hiyo bure kwenye baadhi ya mikoa. 

Pasipo kupoteza muda naomba tukaangalie faida za tohara kiafya kama ifuatavyo; 

1. Usafi, Kikawaida Ngozi ya uume  ( govi) huficha uchafu na pia kuzalisha mafuta meupe meupe yanayojulikana kitaalamu kama smegma ambayo huweka mazingira ya wadudud (bacteria kuzaliana) hivyo kusababisha magonjwa. Hivyo pindi mtu anapofanyiwa tohara huondokana na hatari ya kupata magonjwa hayo ambayo mara nyingi huitwa ni magonjwa ya zinaa. 

2. Hupunguza hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi. 
Mtu anapotahili ngozi ya kichwa cha uume huwa ngumu na kuzuia kupata michubuko kiurahisi tofauti na ya mtu ambaye hajatahili hivyo kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kiasi fulani. Japo ukweli ni kwamba ili upukane na ugonjwa wa huu hatari wa ukimwi unakiwa kuna makini sana kwa kuachana na ngono zembe. 

3. Kufanyiwa tohara ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya saratani ya uume  ( penis cancer) 
utafitiu unaonesha kua saratani ya uume inawapata sana watu ambao hawajatahili 

4. Hupunguza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake. 
Utafiti pia unaonesha kua mwanamke kujamiiana na mtu ambaye hajatahili inamweka kwenye hatari ( Risk ) ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kutokana na uchafu unaotunzwa kwenye govi kuweza kua na Virusi aina ya Human Papilloma Virus (HPV) ambavyo husababisha saratani ya shingo ya kizazi. 

5. Kufanyiwa tohara huleta heshima , hii ni kwa wakubwa wenzangu nadhani watakuwa wameelewa zaidi

Post a Comment

0 Comments