Lehemu (Cholestrol) ni mafuta yanayoongezwa mwilini kupitia chakula na pia hutengenezwa na ini kwa ajili ya utendaji kazi wa mwili kwa ufanisi. Kiwango kizuri cha lehemu (good cholestrol) ni muhimu kwa ajili ya utendaji kazi wa mwili na wakati huo huo kiwango kibaya cha lehemu (bad cholestrol) huweza kuleta madhara makubwa mwilini. Lehemu mbaya (bad cholestrol) huweza kuongeza hatari ya matatizo kama shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na kiharusi. Kuongezeka kwa lehemu mwilini kwa kawaida huwa hakuoneshi dalili yoyote.
Cholestrol husafirishwa na kuingizwa mwilini kupitia proteins. Lehemu zikiungana na protein huitwa Lipoproteins. Kuna aina mbili za lipoproteins:
High Density Lipoproteins (HDL)- Hii huchukua cholestrol kutoka ndani ya seli na kuzipeleka kwenye ini. Ndani yaini huvunjwavunjwa na kuyeyushwa na pengine hutolewa nje ya mwili kama uchafu. Kwa sababu hiyo HDL huitwa lehemu nzuri (good cholestrol). Kwa hiyo kiwango kikubwa cha HDL ni muhimu kwa ajili ya mwili.
Low Density Lipoproteins (LDL)- Hii husafirisha cholestrol na kuzipeleka kwenye seli zenye uhitaji. Kama itakuwa nyingi kwenye seli,lehemu zitaanza kujijenga kwenye kuta za arteri na kusababisha artery kupungua kipenyo (atherosclerosis). Kwa hiyo aina hii huitwa lehemu mbaya (bad cholestrol).
Faida za Cholestrol mwilini:
Baadhi ya faida za lehemu mwilini ni kama: kutengeneza muundo wa cell wall,hutengeneza nyongo (bile) ili kusaidia mmeng'enyo kwenye utumbo mwembamba,huruhusu mwili kutengeneza vitamin D,husaidia mwili kutengeneza baadhi ya homoni.
Chanzo Cha Kuzidi Lehemu (Cholestrol)
1. Mtindo wa maisha
Mtindo wako wa maisha huweza kuongeza hatari ya kupata cholestrol nyingi. Hii ni kupitia:
Chakula- kula chakula chenye mafuta kwa wingi huchangia kuongeza lehemu nyingi mwilini. Vyakula vinavyotokana na ini,figo,nyama,cheese,chocolate,vyakula vya kuokwa,vyakula vilivyosindikwa na mayai huongeza lehemu nyingi mwilini.
Cholestrol husafirishwa na kuingizwa mwilini kupitia proteins. Lehemu zikiungana na protein huitwa Lipoproteins. Kuna aina mbili za lipoproteins:
High Density Lipoproteins (HDL)- Hii huchukua cholestrol kutoka ndani ya seli na kuzipeleka kwenye ini. Ndani yaini huvunjwavunjwa na kuyeyushwa na pengine hutolewa nje ya mwili kama uchafu. Kwa sababu hiyo HDL huitwa lehemu nzuri (good cholestrol). Kwa hiyo kiwango kikubwa cha HDL ni muhimu kwa ajili ya mwili.
Low Density Lipoproteins (LDL)- Hii husafirisha cholestrol na kuzipeleka kwenye seli zenye uhitaji. Kama itakuwa nyingi kwenye seli,lehemu zitaanza kujijenga kwenye kuta za arteri na kusababisha artery kupungua kipenyo (atherosclerosis). Kwa hiyo aina hii huitwa lehemu mbaya (bad cholestrol).
Faida za Cholestrol mwilini:
Baadhi ya faida za lehemu mwilini ni kama: kutengeneza muundo wa cell wall,hutengeneza nyongo (bile) ili kusaidia mmeng'enyo kwenye utumbo mwembamba,huruhusu mwili kutengeneza vitamin D,husaidia mwili kutengeneza baadhi ya homoni.
Chanzo Cha Kuzidi Lehemu (Cholestrol)
1. Mtindo wa maisha
Mtindo wako wa maisha huweza kuongeza hatari ya kupata cholestrol nyingi. Hii ni kupitia:
Chakula- kula chakula chenye mafuta kwa wingi huchangia kuongeza lehemu nyingi mwilini. Vyakula vinavyotokana na ini,figo,nyama,cheese,chocolate,vyakula vya kuokwa,vyakula vilivyosindikwa na mayai huongeza lehemu nyingi mwilini.
Mazoezi- Kukosa mazoezi husababisha kuongezeka kwa hatari ya magonjwa ya moyo. Kufanya mazoezi mara kwa mara husaidia kupunguza lehemu mbaya (LDL) na kuongeza lehemu nzuri (HDL). Mazoezi pia husaidia kupunguza uzito wako. Kusudia kufanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku ili kuweka mwili wako sawa.
Uzito au unene kupita kiasi- Kuongezeka kwa uzito na unene huweza kuongeza cholestrol mbaya (LDL) mwilini na kupunguza cholestrol inayotakiwa mwilini (HDL). Ni chanzo kikubwa pia kwa magonjwa ya moyo.
Kunywa pombe sana- Kiwango kikubwa cha pombe,huongeza cholestrol mbaya (bad cholestrol) mwilini.
Kuvuta sigara- kemikali inayopatikana kwenye sigara inayoitwa acrolein,huzuia lehemu nzuri (good cholestrol-HDL) kusafirisha cholestrol kupeleka kwenye ini na kusababisha cholestrol kujikita kwenye kuta za damu,tatizo lianaloitwa atherosclerosis.
2. Matatizo ya kiafya
Baadhi ya matatizo ya kiafya,huweza kusababisha kuongezeka kwa lehemu nyingi kwenye damu. Matatizo hayo ni kama yafuatayo:
- Shinikizo la juu la damu
- Ugonjwa wa kisukari
- Magonjwa ya ini
- Magonjwa ya figo
- .upungua kwa kiwango cha thyroid (hypothyroidism)
3. Sababu nyinginezo
Sababu zifuatazo huweza kuongeza kiwango kikubwa cha lehemu mwilini. Sababu hizi huweza kuwa:
Historia ya familia ya kuwepo kwa ugonjwa wa coronary
Historia ya kifamilia- Vinasaba vyako huweza kuamua kiasi cha lehemu unachoweza kuwa nacho. Kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu mbaya (LDL) huweza kurithiwa katika familia.
Umri- Kuongezeka umri huweza kuchangia sana kuongeza kiwango cha cholestrol mbaya kwenye damu. Mwanamke ambaye hajakoma hedhi huwa na kiwango sawa cha cholestrol na mwanamume wa rika yake,lakini baada ya kukoma hedhi kiwango cha cholestrol mbaya (LDL) kwa mwanamke huongezeka kuliko hapo kabla.
Asili ya mtu- Watu wa India,Pakistani,Bangladeshi na Sri Lanka wana hatari kubwa ya kuwa na ongezeko kubwa la lehemu kwenye damu.
Madhara Ya Cholestrol Nyingi Mwilini
Madhara ya cholestrol ni mengi na hatarishi sana. Kwa jinsi cholestrol inavyoongezeka mwilini,hujikusanya kwenye kuta za mishipa ya ateri. Cholestrol inapojikusanya kwenye kuta za arteri husababisha hatari ya magonjwa yafuatayo kutokea:
Atherosclerosis- Hili ni tatizo la kupungua kipenyo cha mishipa ya arteri. Hii hutokana na kujikusanya kwa lehemu nyingi kwenye kuta za arteri. Miongoni mwa matatizo yawezayo kutokea kama matokeo ya atherosclerosis ni magonjwa ya moyo na ubongo.
Coronary Heart Disease- Tatizo hili hutokana na kujikusanya kwa cholestrol kwenye kuta za mishipa ya arteri ya coronary inayopeleka damu kwenye moyo.
Angina- Ni aina ya maumivu kwenye kifua yanayotokana na kupungua kwa damu inayoingia kwenye mishipa ya moyo. Angina ni dalili mojawapo ya tatizo la coronary heart disease.
Shambulio la Moyo (Heart Attack)- Ni tatizo litokanalo na hitilafu ya mzunguko wa damu kwenye moyo. Tatizo hili husababisha kufa kwa baadhi ya mishipa ya moyo. Kama tatizo hili halitatibiwa mapeme husababisha kifo mapema sana.
Kiharusi (Stroke)- Ni tatizo linalosababishwa na hitilafu ya mzunguko wa damu kwenye ubongo. Hii hutokana na kuzuiwa kwa damu kupita au kupasuka kwa mshipa wa damu kwenye ubongo.
Ganzi Miguuni- cholestrol ikizidi mwilini husababisha upungufu wa damu kwenye mishipa ya damu miguuni na kusababisha ganzi.
Mawe Kwenye Mfuko Wa Nyongo (Gallstone)- Zaidi ya 80% ya matatizo ya mawe kwenye mfuko wa nyongo husababishwa na kuzidi kwa cholestrol kuliko kiwango cha kawaida.
Jinsi Ya Kudhibiti Cholestrol Mwilini
Mtindo wa maisha kwa ujumla una sehemu kubwa katika kupunguza na kudhibiti kiwango kikubwa cha cholestrol mwilini. Mambo yafuatayo yakifanywa yataweza kukusaidia kupunguza kiwango cha lehemu mwilini mwako:
1. Kula chakula kinachojenga afya ya moyo
Tumia mafuta yasiyo na madhara- Mafuta yatokanayo na wanyama (saturated fats) huongeza cholestrol kwa wingi na LDL pia. MIongoni mwa vyakula vyenye saturated fats ni kama nyama nyekundu,nyama iliyosindikwa na maziwa yaliyosindikwa. Tumia matunda kama parachichi,karanga na almond kwa ajili ya kuongeza HDL.
Dhibiti kiwango cha mafuta unachokula- Vyakula kama mayai,nyama na mafuta ya maziwa husababisha ongezeko la mafuta kwa wingi mwilini mwako. Punguza ulaji wa mayai angalau yasizidi 7 kwa wiki.
Kula nafaka nzima- Vyakula vya nafaka nzima hufaa sana kwa ajili ya afya ya moyo. Kula mkate usiokobolewa,tambi zisizokobolewa,ngano isiyokobolewa na mchele wa brown.
Kula matunda na mboga za majani kwa wingi- Mboga na matunda huwa na nyuzi nyuzi nyingi zinazosaidia kupunguza cholestrol kwa wingi.
2. Punguza uzito wako- Ongezeko la uzito wako huchangia kuongezeka kwa cholestrol kwa wingi.
3. Fanya mazoezi mara kwa mara- Mazoezi husaidia kupunguza kiwango chako cha cholestrol. Kufuatana na ushauri wa daktari wako,dakika 30 hadi 60 hivi ni muhimu kwa ajili ya afya yako. Wakati fulani kama huwezi kufikisha muda huo wa mazoezi,fanya hata kidogo. Unaweza kufanya mazoezi kwa njia ya kukimbia,kuendesha baiskeli au kuogelea. Mazoezi kidogo ni bora kuliko kukosa mazoezi kabisa.
4. Epuka kuvuta sigara- Uvutaji wa sigara ni hatari sana kwa afya ya moyo. Hii ni kwa sababu sigara husababisha hatari ya kutokea plaque kwenye kuta za arteri. Kama unavuta sigara acha,ili kutunza afya yako.
Ni Matumaini yangu ndugu msomaji kuwa umeongeza maarifa ya kutosha kuhusiana na Cholestrol (lehemu). Kwa leo tutaishia hapa,endelea kufuatana nasi katika mada zitakazofuata.




0 Comments