Aliendelea ” Malkia. Nimesikia sifa zako nyingi katika medani, sifa zake katika operesheni mbalimbali. Uwezo wako huo katika sifa nilizozisikia ndizo zimekufanya uwe huru leo. Kwa ajili ya kuja kupambana. Kufanya kazi. Kufanya biashara. Biashara ya kifo. Nakuamini sana Malkia usiniangushe” Don Genge alisema kwa nguvu macho yakiwa kwa Malkia.
Sasa sura yake aliigeuzia kwa Peter
“Peter Kissali Mwendawazimu, najua wewe ni kichwa sana. Uko vizuri sana katika kupanga mambo, uko vizuri katika kuitumia akili yako. Wewe ni genius, na mipango kama hii inahitaji mageneniuos kama wewe. Kwa kutumia akili zako naomba tuifanye hii misheni na kuikamilisha”
Sasa alimwangalia Malolo huku akiongea ” Malolo, naujua uwezo wako katika mapambano. Najua na hii biashara itahitajika mapambano. Mapambano ya nguvu. Najua mauaji niliyoyafanya juzi yatawasogeza wambea kadhaa hapa, akiwemo Daniel Mwaseba. Malolo upo huru mahsusi kwa ajili ya kuitoa roho ya Daniel Mwaseba. Na naamini utafanikisha hilo”
“Bila shaka mkuu” Malolo alijibu kwa kujiamini.
Don Genge aliongea ” Safi sana Malolo. Sasa tufanye hii kazi jamani. Ni kazi ya mwaka mmoja tu ambayo na uhakika tukiimaliza itawaacha wote kuwa mabilionea. Hamtakuwa na haja ya kusaka pesa tena katika maisha yenu, mtakuwa na pesa za kutumia hadi mnakufa”
Wote watatu walitabasamu. Wote walikuwa wapenda pesa, na walikuwa wametajiwa pesa za kutosha. Iliwalazimu kutabasamu.
“Kuna yeyote mwenye maoni, swali, dukuduku, ama ushauri? Wakati ni huu” Don Genge aliuliza huku akihangaika kuitoa sigara yake mfukoni.
Mimi nina swali dogo tu, lakini muhimu katika operesheni yoyote ile, je kuna zana za kutosha kuifanya hii kazi?” Malkia aliuliza huku akimwangalia Don Genge.
“Tuna zana za kutosha. Tuna kila kila kitu kinachoweza kutufanya tufanye hii kazi kwa asilimia mia moja. Tuna silaha nyingi, tena za kisasa. Tuna Proxine za kutosha, ambazo tone moja tu huruhusu ngozi kuvuka mwilini mithili ya kanzu. Tuna magari mengi ya kutupeleka hapa na pale, ndege binafsi. Tuna rasilimali watu makini ambao ni nyinyi. Hatuwezi kujitetea kwa kushindwa hii kazi eti kutokana na kutokuwa na zana” Don Genge alielezea kwa kirefu.
Wote waliitikia kwa kichwa.
“Swali lengine?” Don Genge aliwauliza tena.
“Mimi nina ushauri. Yatupasa kuongeza watu ili kuweza kuifanya hii kazi kwa haraka na ufanisi. Ngozi elfu kumi zinazohitajika ni nyingi sana. Kwa wastani yatupasa tuue watu ishirini na saba kwa siku. Ni watu wengi sana hao. Maana hapo kwa sisi watatu kila mmoja yampasa kuua watu tisa kwa siku. Its not easy task Don. Nashauri tuongeze watu” Peter alieleza.
“Kuongeza watu sio tatizo, tatizo ni kuwapata watu wanaojua kufanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa kama nyinyi. Kama mnao hao watu, nipeni sifa zao nione kama tunaweza kuwajumuisha katika operesheni hii. Ila ni lazima wajue namna ya kutunza siri na kufanya kazi bara’bara ” Don Genge alijibu.
Wote watatu waliangaliana usoni. Walikaa kimya, ishara kwamba hawakuwa na mtu.
TWENDENI TU…TUUSOME HUU MCHEZO..
ITAENDELEA

0 Comments