Kiwiliwili cha mzee Mwamaja, kiwiliwili kisicho na mguu mmoja, kiwiliwili kisicho na kichwa kilikuwa kimesweka vibaya katika kona nyingine ya selo. Inspekta John aligeuza sura yake kuangalia kona nyingine. Alimuona mhalifu mpya akiwa amejikunyata konani, mwili wake wote ukiwa umetapaa damu.
Inspekta John alirudia tena kutazama kona moja baada ya nyingine ya ile selo. Aliviona vitu vilevile alivyoviona awali. Inspekta alikuwa bado haamini kilichotokea.
“Kumetokea nini humu? Vitu kama hivi vinatokeaje ndani ya kituo cha Polisi? Mauaji ya kinyama kama haya yanawezaje kutokea ndani ya selo, selo ya Polisi?
Polisi walikuwa wapi? Muuaji aliingiaje hadi ndani ya selo? Muuaji alitokaje ndani ya eneo la Polisi?” Inspekta John alijiuliza kimoyomoyo. Lakini hakupata majibu. Hakutaka kujisumbua kujiuliza mwenyewe, alimuona wa kumjibu maswali yake yote, ambaye bila shaka alikuwepo wakati mauaji yale yakifanyika, na yeye alibaki hai. Na aliamua kwenda kumuuliza.
Alianza kumsogelea Mhalifu yule ili amjibu maswali mengi na magumu yakiyokisumbua kichwa chake. Kila alipopiga hatua kuelekea katika kona aliyekuwepo yule mhalifu mpya. Ulitokea utata!
Jamaa alipiga kelele kali kila hatua ya Inspekta John ilivyokuwa inagusa sakafu ya selo.
Ilikuwa kelele! Kelele nyingi! Kelele zisizo na kifano!
Hatua za Inspekta John zilikuwa kama zinamtonesha yule mhalifu katika vidonda vyake…
“Kimetokea nini humu?” Safari hii sauti ya Inspekta John iliweza kutoka nje ya mdomo wake, na kusikiwa na askari wote waliokuwepo pale mlangoni.
Lakini hakuna aliyemjibu.
Inspekta John aliendelea kupiga hatua taratibu kumfata yule mhalifu mtukanaji, mhalifu anayepiga makelele kila hatua ya Inspekta John ilivyokuwa inagusa chini. Safari hii ilikuwa vilevile, kila Inspekta John alivyogusa ardhi ndipo makelele toka kwa yule mhalifu yalivyokuwa yanazidi.
Inspekta John alisimama.
Aligeuka mlangoni, lakini macho yake yalienda moja kwa moja nyuma ya mlango. Aliona kitu! Utumbo wa binadamu ulikuwa umekusanywa hovyo nyuma ya mlango wa selo.
Bila kupenda Inspekta John lilimtoka tusi zito la nguoni. Sasa alijua kwamba mle selo aliingia muuaji katili sana. Muuaji anayejisikia raha kuua. Muuaji aupendao mchezo wa mauaji.
Muda huohuo baada ya kuuona tu ule utumbo ndipo alipoanza kuivuta harufu mbaya mle ndani.
Harufu ya utumbo!
Harufu ya damu!
Damu ya binadamu!
Hakuweza kuivumilia. Alitoka nje harakaharaka.
Aliwakuta askari wakimsubiri kwa nje.
“Kumetokea nini kwani humu ndani?” Inspekta John aliuliza tena swali lilelile.
Askari wale watatu waliangaliana usoni, hakuna aliyemjibu. Waliendelea kukaa kimya. Sura zao zikiwa na hofu.
Inspekta John akauliza swali lengine ” Ni nani aliyenipigia simu nilipokuwa ofisini?”
Askari wote walikataa kwa mabega.
“Nyinyi Askari!” Inspekta John aliita kwa nguvu.
Wote walisimama imara! Wakimuangalia Inspekta John kwa sura zenye uwoga.
“Nani aliyenipigia simu?” Inspekta John aliuliza tena.
“Sijui” Wote walijibu kwa pamoja.
“Nani alikuwa zamu hapa usiku?”
Askari wawili walimuonesha askari mwenzao kwa kidole.
“Nakuhitaji ofisini” Inspekta John alisema huku akiongea.
Alitembea kama hatua tatu. Akasimama. Akageuka nyuma, aliongea tena “Mpigieni daktari akishafanya mambo yake pigeni picha kila kitu kilivyo humu ndani. Then muite wahudumu wasafishe, na huyo jamaa mpelekeni hospitali. Kuweni makini lakini”
“Sawa afande” Askari wale wawili waliobaki waliitikia kwa pamoja.
Katika viti viwili vilivyokuwepo ofisini kwa inspekta John vilikuwa vimekaliwa na askari wawili. Kimoja kilikaliwa na Inspekta John mwenyewe na kingine kilikuwa kimekaliwa na askari mrefu mweusi. Alikuwa anajulikana kwa jina la afande Frank. Askari aliyekuwa zamu jana usiku.
Inspekta John alimwangalia kwa muda yule askari aliyekuwa mgeni pale kituoni. Kisha aliongea kwa sauti kavu.
“Nambie nini kilitokea jana usiku?”
Afande Frank alikaa vizuri kitini huku akiongea “Afande mimi hata sielewi”
“Nakuuliza kwa mara ya pili. Kilitokea nini jana usiku?” Inspekta John aliongea huku akielekea kuufunga mlango kwa ndani.
Afande Frank aliogopa sana. Alishazisikia sifa za Inspekta John tangu siku ya kwanza tu alipohamia katika kituo cha Polisi Mbozi. Kwamba hapendi utani. Hataki mas’hara katika kazi. Anaweza kukufanya lolote lile ukitaka kumuharibia kazi. Sasa kufungwa kwa mlango ilidhihirisha hali ya hatari kwake.
Alijikuta akiropoka kwa sauti yenye kihoro ” Afande nahisi kuna njama hapa kituoni”
Inspekta John alikuwa anarudi kitini kutokea kule mlangoni
“Njama? Njama kivipi?” Alimuuliza akiwa anarejea kukaa kitini.

“Njama? Njama kivipi?” Alimuuliza akiwa anarejea kitini.
ITAENDELEA

0 Comments